Kindi ni wanyama wadogo wa familia Sciuridae. Spishi nyingine huitwa kidiri au kuchakulo. Wanatokea Amerika, Ulaya, Asia na Afrika na wamewasilishwa katika Australia. Takriban spishi zote huishi mitini, lakini kuchakulo huishi ardhini. Mkia wa kindi una urefu karibu na ule wa mwili, pengine zaidi. Hula mbegu, makokwa, matunda, nyoga, matumba na machipukizi. Wakati ambapo chakula cha kimea ni adimu, kindi hula chakula cha kinyama pia, k.f. wadudu, mayai, ndege wadogo, makinda ya nyoka na wagugunaji wadogo. Spishi kadhaa za tropiki hula wadudu kushinda chakula cha kimea.