dcsimg

Mkuyu ( Suaíli )

fornecido por wikipedia emerging languages

Mikuyu ni miti ya jenasi Ficus. Kwa kawaida hii ni miti mikubwa. Maua, na kwa hivyo matunda pia, huota kutoka shina na matawi makubwa. Matunda huitwa makuyu. Mkuyu unaopandwa na ambao matunda yake huliwa sana, una jina lake: mtini, na matunda yake matini. Kuna kadiri ya spishi 800 za mikuyu.

Makuyu siyo matunda kwa kweli. Tabaka la nje ni sehemu ya tawi iliyojifunga katika tufe na huitwa sikonio (syconium). Mkabala na kikonyo kuna tundu dogo liitwalo ostioli. Maua yapo upande wa ndani wa ukuta wa sikonio. Uchavushaji wa maua hufanyika na nyigu wadogo sana (nyigu-makuyu). Jike la nyigu, ambao ametoka kwenye sikonio nyingine na amepambwa na chavua, aingia kupitia tundu dogo kwa nguvu akipoteza mabawa yake. Halafu ataga mayai katika ovari za maua na sawia achavusha stigma. Baada ya kutoka kwenye mayai lava wala tishu za maua. Madume wakiwa wamekuwa wapevu hawana mabawa na wapanda majike tu. Halafu watoboa tundu katika sikonio ili kuacha majike watoke na baadaye madume wafa. Kila spishi ya mkuyu ana spishi yake (au zake) ya(za) nyigu maalum.

Spishi zilizochaguliwa

Picha

licença
cc-by-sa-3.0
direitos autorais
Waandishi wa Wikipedia na wahariri
original
visite a fonte
site do parceiro
wikipedia emerging languages

Mkuyu: Brief Summary ( Suaíli )