dcsimg

Nge-mjeledi ( Svahili )

wikipedia emerging languages tarafından sağlandı

Nge-mjeledi (kutoka Kiingereza whip scorpion) ni arithropodi wa oda Thelyphonida katika ngeli Arachnida wafananao na nge wa kawaida. Kama hawa wana miguu minane na pedipalpi zenye gando. Mjeledi wa jina lao ni aina ya mkia mrefu na mwembamba. Kama kawaida kiwiliwili chao kina sehemu mbili: kefalotoraksi (cephalothorax: kichwa na kidari) na fumbatio zilizoungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija. Nge-mjeledi wana macho manane, mawili mbele ya kefalotoraksi na matatu kwa kila upande wa kichwa. Pedipalpi zao zinafanana na zile za nge, lakini zina mwiba nyuma ya gando na maneno magumu kwa kitako chao ambayo hutumika kwa kukamua mawindo. Miguu sita tu hutumika kwa kutembea. Jozi ya kwanza imekuwa mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Nge-mjeledi hawana sumu lakini wana matezi yanayotoa mchanganyiko wa asidi ya asetiki na asidi ya kapriliki wakisumbuliwa. Hula arithropodi wengine, pengine nyungunyungu na makonokono uchi pia.

Picha

WikiLettreMini.svg Makala hii kuhusu "Nge-mjeledi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili whip scorpion kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni nge-mjeledi.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

lisans
cc-by-sa-3.0
telif hakkı
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Nge-mjeledi: Brief Summary ( Svahili )