dcsimg

Nyegere ( Svahili )

wikipedia emerging languages tarafından sağlandı

Nyegere, melesi au mhilu (Mellivora capensis) ni mnyama mdogo wa familia Mustelidae anayetokea Afrika, Mashariki ya Kati na Uhindi.

Nyegere huishi peke yao kwenye shimo analolichimba yeye mwenyewe. Ni wachimbaji wazuri sana. Vile vidole vyao vyenye kucha ndefu na ngumu humsaidia sana kwenye kazi hii. Hata kama ardhi ni ngumu sana, ana uwezo wa kuchimba shimo linalomtosha kujificha katika kipindi kinachokadiriwa kuwa ni dakika kumi tu.

NYEGERE (Honey burger) a.k.a "The fearless animal" TABIA NA MAMBO YAKE MENGINE Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii. Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya Ni mnyama mdogo anayekula nyoka, kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k...kwa kifupi anakula kila kitu na ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake. Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe. .Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti. Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake. Wanapatikana India,Kusini magharibi barani Asia na Afrika.

Crystal Clear app babelfish vector.svg Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyegere kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
lisans
cc-by-sa-3.0
telif hakkı
Waandishi wa Wikipedia na wahariri