Kereng'ende ni ndege kadhaa wa jenasi Francolinus katika familia Phasianidae. Huitwa kwale pia pamoja na spishi nyingine za Francolinus. Rangi yao ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Ngozi ya koo na pande zote za macho ni kichele na ina rangi ya manjano, ya machungwa au nyekundu. Huonekana zaidi kuliko spishi nyingine za kwale. Chakula chao ni mbegu, wadudu na nyungunyungu. Hutaga mayai matatu hadi nane ardhini pengine juu ya manyasi makavu.
Spishi zote zinatokea Afrika.