Dudumizi ni ndege wakubwa kadiri wa jenasi Centropus, jenasi pekee ya nusufamilia Centropodinae katika familia Cuculidae. Wana macho mekundu na mkia mrefu, na ukucha wa kidole kikabilicho nyuma ni mrefu sana. Jina “Centropus” linatoka maneno ya Kiyunani: κεντρον = mwiba na πους = mguu. Spishi nyingi zina mabawa kahawianyekundu na kichwa cheusi. Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka na wanyama wadogo, na mayai, makinda, matunda na mizoga pia. Tago lao hujengwa katika uoto mzito na mara nyingi juu yake imefungwa. Jike hutaga mayai 2-5, lakini dume, ambaye ni mdogo zaidi, huatamia na hutunza makinda.