Chawa ni wadudu wadogo wa oda Phthiraptera katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa), lakini hata kama wahenga wao walikuwa na mabawa, chawa hawanayo. Wadudu hawa wote ni vidusia wa nje juu ya ndege na mamalia isipokuwa Monotremata (kinyamadege na mhanganungu), popo, nyangumi, pomboo na kakakuona. Kuna aina mbili za chawa: wanaokula nywele, manyoya na seli za ngozi zilizokufa, na wanaofyunza damu ya mwenyeji. Chawa wa aina ya kwanza wana vipande vya mdomo vya kutafuna, wale wengine wana mdomo wa kufyunza. Miguu inabeba aina za magando madogo ili kushika nywele au manyoya ya mwenyeji. Kwa kawaida mayai ya chawa yamegandia nywele au manyoya, au pengine yamewekwa ndani ya shina la unyoya.
Chawa wanaopatikana kichwani hawana magonjwa yoyote wanayosababisha lakini waliye mwilini huwa wanasababisha magonjwa. Hata hivyo, katika jamii nyingi, chawa huonekana kana kwamba huwasumbua walio wachafu ama wanaoishi kwa uchafu. Pia hufanya mtu adhoofike kwa sababu ya kunyonywa na vidusia hawa.
Kuna dawa kadhaa za kupuliza ili kuwaua wadudu hawa. Usafi pia ni muhimu kama wataka kuwakwepa.