Sokwe mkubwa au sokwe peke yake ni jina la binadamu na nyani wakubwa wa familia Hominidae wanaofanana sana na binadamu. Tofauti na nyani wengine ni kuwepo kwa mkia; karibu nyani wote huwa na mkia lakini masokwe wakubwa hawana kabisa. Binadamu (Homo) anahesabiwa pia kama jenasi yenye spishi moja katika familia hii.
Masokwe wasiokuwa wanadamu wanaishi katika maeneo ya tropiki ya Afrika (masokwe mtu na ngagi) na Asia (orangutanu). Wote ni wakazi wa misitu ila tu masokwe mtu wanaoingia pia kwenye mbuga au savana. Wanadamu wanaishi duniani kote kwa kubadili mazingira yao, kuvaa nguo na kujenga majumba yanayowalinda kutoka joto kali ama baridi.
Orangutanu (wa Sumatra) ni sokwe aliyezoea miti zaidi