Nyuki-asali ni aina za nyuki wa kabila Apini katika familia Apidae ambao hutengeneza asali na kuiweka katika sega za nta.
Nyuki-asali hufugwa sana kila mahali duniani lakini wengine wanaishi porini na asali yao hukusanywa kwa kuvunja mizinga yao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki asali wa porini lakini ufugaji nyuki unaendelea kupanuka.
Wadudu wa kijamii
Nyuki-asali ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika makundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga wa nyuki na humu hutunza asali yao.
Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi hili nao ni:
- malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutaga mayai pekee
- nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama kukusanya mbelewele na mbochi, kusafisha mzinga, kutengeneza nta, kujenga sega, kumlisha malkia na majana, kulinda mzinga
- nyuki wa kiume au wadudume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kumpanda malkia ambaye si yule wa mzinga wake kwa kawaida; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena
Spishi na nususpishi za Afrika
-
Apis mellifera
-
Apis m. adansonsii, Nyuki-asali wa Adanson
-
Apis m. capensis, Nyuki-asali kusi
-
Apis m. intermissa, Nyuki-asali mweusi
-
Apis m. jemenitica, Nyuki-asali wa Pembe la Afrika
-
Apis m. lamarckii, Nyuki-asali wa Lamarck
-
Apis m. litorea, Nyuki-asali pwani
-
Apis m. major, Nyuki-asali wa Maroko
-
Apis m. monticola, Nyuki-asali milimani
-
Apis m. nubica, Nyuki-asali wa Sudani
-
Apis m. sahariensis, Nyuki-asali jangwani
-
Apis m. scutellata, Nyuki-asali wa Afrika
-
Apis m. unicolor, Nyuki-asali wa Madagaska
Spishi za Asia
Picha
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni
mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu
Nyuki-asali kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari.