dcsimg

Mbwa ( swahili )

fourni par wikipedia emerging languages

Mbwa ni wanyama mbua wa familia Canidae, lakini takriban spishi zote za Afrika zinaitwa bweha au mbweha.

Ukubwa wa spishi za mwitu unatofautiana kutoka 24 sm (fenek) mpaka 2 m (mbwa-mwitu wa Ulaya (kadiri ya vipimo kwa mbwa-kaya ni 9.5-250 sm).

Mbwa wa familia Canidae hupatikana mabara yote isipokuwa Antaktika.

Wanyama hawa wana pua ndefu na miguu mirefu na mkia wa manyoya. Rangi yao ni kijivu, kahawia au hudhurungi; kwa kawaida tumbo ni jeupe.

Spishi nyingine zinatokea misituni na nyingine zinatokea maeneo wazi. Mbwa hukamata mawindo aina yoyote lakini ukubwa wa mawindo unafuatana na ukubwa wa spishi ya mbwa. Hata hivyo, spishi zinazoishi kwa makundi, kama mbwa-mwitu wa Afrika, zinaweza kukamata windo kubwa sana kuliko wao wenyewe. Spishi kadhaa hufugwa na binadamu, hususan mbwa-kaya.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha

Viungo vya nje

licence
cc-by-sa-3.0
droit d’auteur
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Mbwa: Brief Summary ( swahili )