Viluwiri ni ndege wa jenasi mbalimbali za familia ya Rallidae. Spishi za jenasi Rallus zinaitwa kibilinzi pia. Viluwiri wa Afrika wana rangi zilizofifia na hawaoneki rahisi wotoni, lakini husikika mara zaidi. Wana domo refu, miguu myembamba na vidole virefu. Spishi nyingi zaidi zinatokea karibu na maji, mabwawani au nyikani majimaji ambapo hula wadudu na wanyama wadogo wa maji na wa matope. Kwa kawaida tago lao limefanyika kwa mimea ya maji kwa umbo wa bakuli mahali pakavu katika bwawa na huyataga mayai 2-12.