Koikoi ni ndege wakubwa wa jenasi Ardea katika familia ya Ardeidae wenye miguu mirefu na domo refu na nyembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Spishi zenye rangi ya kahawiachekundu huitwa pondagundi pia. Spishi nyingine nyeupe kabisa inaitwa msuka. Zamani ilikuwa imeainishwa ndani ya jenasi Egretta. Koikoi hupenda kula samaki lakini hula wanyama wadogo pia, kama vyura, mijusi na nyoka. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti. Jike huyataga mayai 2-6.