Vipozamataza ni ndege wadogo wa familia Alaudidae; spishi nyingine zinaitwa tuju au kindoro. Takriban spishi zote zina rangi ya kahawa na michirizi myeusi. Hawa ni ndege wa nyanda, spishi kadhaa tu zinapatikana misituni. Wanatokea mabara yote isipokuwa Amerika; spishi moja tu imefika huko. Hula mbegu hasa na wadudu pia. Madume huimba vizuri sana ili kuvutia majike na kuhadharisha madume mengine. Tago lao ni kikombe cha manyasi ardhini na jike huyataga mayai 2-6.