Wadudu siku-moja ni wadudu wa oda Ephemeroptera (ephemeros = -a muda mfupi, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wadudu hawa huishi majini baridi katika muundo wa nayadi (lava ya wadudu wa maji) kwa muda wa mwaka mmoja, halafu hutoka kwenye maji na kuambua mara mbili na kuwa mdudu aliyekomaa wenye mabawa. Licha ya jina lao wadudu waliokomaa huishi muda wa nusu saa hadi siku kadhaa. Wanajamiiana tu na kutaga mayai; hawali na kwa hiyo wana alama za vipande vya mdomo tu na utumbo umejaa na hewa. Kinyume na wadudu waliokomaa nayadi hula viani na diatomea, na spishi kadhaa hula lava za wadudu wengine wa maji.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.