Mabata-bahari ni ndege wa maji wa nusufamilia ya Merginae katika familia ya Anatidae. Mabata hawa wanaishi baharini hasa nje ya majira ya kuzaa. Wengi wana tezi za chumvi maalum ambazo zinawawezesha kuvumilia maji ya bahari. Mabata-domomeno hupenda zaidi mazingira ya mito.
Mabata-bahari hula samakigamba na gegereka wa chini ya bahari. Mabata-domomeno hula samaki. Meno ya madomo yao yanawasaidia kushika mawindo. Takriban spishi zote zinatokea kanda za kaskazini mbali.