Wadudu mabawa-potwa ni wadudu wadogo wa oda Strepsiptera (strepsis = iliyopotwa, ptera = mabawa) wenye mabawa yaliyopotwa. Wadudu hawa ni wadusia wa wadudu wengine, kama nyuki, nyigu, sisimizi, warukaji-majani, mende, panzi na visamaki-fedha.
Madume ya wadudu hawa wana mabawa, miguu, macho na vipapasio kama wadudu wengine, lakini majike wanafanana na lava bila viungo hivi (neotenia, Kiing. neoteny). Majike wanakaa katika mdudu ambamo wamezaliwa. Wanatoa kichwa na protoraksi nje ya mwenyeji ili kumrahisishia dume apande jike.
Kuna familia 7 na spishi 110 katika Afrika.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.