dcsimg

Furukombe wa Afrika ( swahili )

fornì da wikipedia emerging languages

Furukombe, fukombe, kwazi, yowe au tai mlasamaki (Haliaeetus vocifer[1]) ni spishi mkubwa wa tai. Yeye ndiye ndege wa kitaifa wa nchi za Zimbabwe na Zambia.

Ndege anayefanana naye zaidi ni Furukombe wa Madagaska (H. vociferoides) ambaye yumo hatarini sana kuangamizwa. Kama tu tai wote wa bahari wenye aina mbili maalum, huyu ana spishi mwenye kichwa cheupe (Furukombe) na mwingine mwenye kichwa cha hudhurungi. Hawa ni ndege wa zamani sana, na kwa hivyo wao huwa na makucha, midomo, na macho ya rangi nyeusi (Wink na wengineyo, 1996). Spishi wote wawili wana angalau mikia yenye rangi nyeupe, ikiwemo hata makinda.

Sifa

African fish eagle flying cropped.jpg
African fish eagle from front flying.jpg
 src=
Yai la furukombe wa Afrika

Furukombe ni ndege mkubwa, na ule wa kike ana uzani wa kilo 3.2-3.6 (paundi 7-8) na ni mkubwa kuliko ule wa kiume ambaye ana uzani wa 2-2.5kg (paundi 4.4-5.5). Ndege wa kiume kawaida huwa na mabawa yenye upana wa mita 2 (futi 6), huku ndege wa kike wakiwa na mabawa yenye upana wa mita 2.4 (futi8). Urefu wao ni sentimita 63-75 (incha 25-30). Wao huweza kutofautishwa rahisi sana na ndege wengine huku miili yao ikiwa ya rangi ya kahawia, na mabawa yao meusi huwa na nguvu nyingi. Kichwa, kifua na mkia ya furukombe wote ina rangi nyeupe kama theluji na mdomo uliojipinda, ambao mara nyingi ni wa rangi ya samawati lakini ncha yake huwa nyeusi.

Wanapopatikana

Spishi huyu mara nyingi kupatikana katika maziwa yenye maji yasiyokuwa na chumvi, mabwawa ya maji, au mito ingawa wakati mwingine wao huweza kupatikana karibu na pwani katika maeneo ambapo mito inaingia baharini. Furukombe wana asili yao Barani Afrika, huku wakipatikana katika maeneo makubwa ya Afrika ya upande kusini mbele ya ncha ya chini ya Jangwa la Sahara.

Kuzaana

Msimu wa kuzaana wa furukombe ni wakati wa msimu wa kiangazi, wakati ambapo viwango vya maji vimepungua. Furukombe huaminika kuendelea na shughuli za kuzaana maisha yao yote, na furukombe wawili mara nyingi huwa na viota viwili wanayvovitumia tena na tena. Kwa sababu viota vyao mara nyingi hutumika tena na tena na kuboreshwa kupitia kipindi cha miaka mingi, vinaweza kuwa vikubwa sana, huku vingine vikifikia mita 2 (futi sita) kwa upana na mita 1.2 (futi 4) kwa undani. Viota vyao hujengwa katika mti mkubwa na hujengwa mara nyingi kwa kutumia vijiti na vipande vingine vya mbao.

Furukombe wa kike hutaga kati ya yai 1 au 3, ambayo ni meupe na yenye madoadoa mekundu. Mayai hulaliwa na furukombe wa kike, lakini ndege wa kiume atayalalia mayai wakati ndege wa kike anapoenda kuwinda. Mayai huchukua muda wa kati ya siku 42 na 45 kuanguliwa. Mayai mara nyingi yataanguliwa siku tofauti, na makinda wa kwanza kawaida atawauwa wowote watakaozaliwa baada ya yeye. Makinda hukomaa baada ya siku 70 hadi 75, na baada ya wiki 8 makinda atakuwa tayari kujuilisha na kawaida huanza kutoka nje yak iota baada wiki 2 baadaye.

 src=
Furukombe mara nyingi husimama mitini huku miili yao ikiwa wima vilivyo.

Lishe

Furukombe mara nyingi hula samaki, ambao, anapowaona kutoka mtini aliposimama, anashuka chini haraka na kuwanyakua kutoka majini kwa kutumia makucha yake makubwa na kupaa juu tena kumla samaki Yule. Ikiwa furukombe atampata samaki mwenye zaidi ya uzani 1.8 (paudni 4) atakuwa mzito sana kuruhusu kupaa angani, kwa hivyo atamvuruta majini hadi afikie ufuo wa maji. Ikiwa samaki ni mzito kiasi kwamba hawezi kupaa kabisa, atamuangusha majini na kuelekea hadi ufuo ulio karibu zaidi. Pia samaki Yule hula ndege wa majini, mamba wachanga na mizoga.

Ishara

Picha za ndege katika nembo ya Namibia.

Marejeo

  • BirdLife International (2004). Haliaeetus vocifer. 2006. IUCN Red List of Threatened Species. IUCN 2006. www.iucnredlist.org. Retrieved on 12 Mei 2006. Database entry includes justification for why this species is of least concern
  • Wink, M.; Heidrich, P. & Fentzloff, C. (1996): A mtDNA phylogeny of sea eagles (genus Haliaeetus) based on nucleotide sequences of the cytochrome b gene. Biochemical Systematics and Ecology 24: 783-791. PDF fulltext
  • Tanzaniabirds.net: African fish eagle

Maelezo chini ya ukurasa

  1. Asili ya jina: Haliaeetus, kutoka Kilatini, maana "tai wa bahari"; vocifer, kutoka neno la Kilatini vox, "sauti", + -fer, kiumbe anayebeba kitu fulani, ili kuashiria kelele zinazofanywa na ndege huyu anapoita. Sauti hizi, wakati anapokaa, hutolewa huku kichwa kikiwa kimeinamishwa nyuma kabisa, jambo ambalo si la kawaida katika tai wa bahari isipokuwa katika spishi hii na ile ya Madagaska (furukombe Malagasi).
licensa
cc-by-sa-3.0
drit d'autor
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Furukombe wa Afrika: Brief Summary ( swahili )

fornì da wikipedia emerging languages

Furukombe, fukombe, kwazi, yowe au tai mlasamaki (Haliaeetus vocifer) ni spishi mkubwa wa tai. Yeye ndiye ndege wa kitaifa wa nchi za Zimbabwe na Zambia.

Ndege anayefanana naye zaidi ni Furukombe wa Madagaska (H. vociferoides) ambaye yumo hatarini sana kuangamizwa. Kama tu tai wote wa bahari wenye aina mbili maalum, huyu ana spishi mwenye kichwa cheupe (Furukombe) na mwingine mwenye kichwa cha hudhurungi. Hawa ni ndege wa zamani sana, na kwa hivyo wao huwa na makucha, midomo, na macho ya rangi nyeusi (Wink na wengineyo, 1996). Spishi wote wawili wana angalau mikia yenye rangi nyeupe, ikiwemo hata makinda.

licensa
cc-by-sa-3.0
drit d'autor
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Африк нөмрөг бүргэд ( mòngol )

fornì da wikipedia emerging languages

Африк нөмрөг бүргэд (Haliaeetus vocifer[2]) нь Харцагынхан овгийн махчин шувуу юм. Энэхүү шувуу нь Зимбабве, Замби улсын үндэсний шувуу болно.

Гадаад төрх

African fish eagle flying cropped.jpg
African fish eagle from front flying.jpg
 src=
Haliaeetus vocifer

Энэхүү томхон бүргэдийн эмэгчин нь 3.2-3.6 кг, эрэгчин нь 2-2.5 кг жинтэй. Далавчаа дэлгэхэд эрэгчин 2 м орчим, эмэгчин 2.4 м байна. Биеийн урт 63–75 см. Бие нь бор, том хүчирхэг далавч нь хар өнгөтэй. Толгой, цээж, сүүл нь цасан цагаан ба хошуу нь хар үзүүртэй шар байдаг.

Тэд Африк тивийн цэнгэг уст гол мөрөн, нуурын орчмоор нутаглана.

Үржил

Тэдний үржлийн улирал усны түвшин намссан хуурай улиралд болдог. Энэхүү бүргэд нь нэг хостойгоо үхэн үхтлээ амьдардаг аж. Хосууд 2 ба түүнээс дээш үүртэй байх ба сэлгэн амьдарна. Жил бүр засаж сэлбэсээр зарим хуучин үүр 2 м голчтой, 1.2 м хүртэл өндөртэй болсон байдаг. Томхон модон дээр мөчир зэргээр үүр засаж 1-3 өндөг гаргана. Голдуу эмэгчин нь өндгөө дарах ба хааяа эмэгчинг анд гарсан үед эрэгчин дардаг.

42-45 хоноод өндөг хагарж ангаахай гарч эхлэх ба хамгийн анх төрсөн нь хэдэн өдрийн дараа гарсныгаа алж хороодог ажээ.

Hvidhovedet afrikansk ørn2.png

Идэш тэжээл

Гол идэш нь загас бөгөөд модны мөчир дээр суун хүлээж байгаад загас өнгөрмөгц шүүрэн барьдаг. Мөн жижиг яст мэлхий, матрын зулзага, ягаан нал болон улай сэг иддэг аж.

Эшлэл

  1. BirdLife International (2005). Haliaeetus albicilla. 2006. Байгаль Хамгаалах Олон Улсын Холбооны Ховордсон амьтдын улаан жагсаалт. IUCN 2006. www.iucnredlist.org. 24 August 2006-д авсан. Database entry restates that the White-tailed Eagle has been downlisted to Least Concern in 2006.
  2. Etymology: Haliaeetus, New Latin for "sea-eagle". vocifer, from Latin vox, "voice" + -fer, one who bears something, in allusion to the conspicuous yelping calls. These are, when sitting, given with the head fully thrown to the back, a peculiarity found among sea-eagles only in this and the Madagascar species.

licensa
cc-by-sa-3.0
drit d'autor
Wikipedia зохиогчид ба редакторууд

Африк нөмрөг бүргэд: Brief Summary ( mòngol )

fornì da wikipedia emerging languages

Африк нөмрөг бүргэд (Haliaeetus vocifer) нь Харцагынхан овгийн махчин шувуу юм. Энэхүү шувуу нь Зимбабве, Замби улсын үндэсний шувуу болно.

licensa
cc-by-sa-3.0
drit d'autor
Wikipedia зохиогчид ба редакторууд