dcsimg

Nge-mjeledi mkia-mfupi ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Nge-mjeledi mkia-mfupi (kutoka Kiing. short-tailed whip scorpion) ni arithropodi wa oda Schizomida katika ngeli Arachnida wanaofanana na nge-mjeledi wadogo. Wengi sana wana urefu wa chini ya mm 5. Kama arakinida wengine kiwiliwili chao kina sehemu mbili: kefalotoraksi (cephalothorax) na fumbatio. Sehemu hizi zimeungwa kwa pediseli (pedicel) nyembamba kwa umbo wa mrija kama kwa buibui. Mwisho wa fumbatio una mkia mwembamba mfupi. Kefalotoraksi imefunika juu kwa magamba.

Wadudu hawa wana miguu minane kama arakinida wote, lakini jozi ya kwanza ni mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Jozi ya mwisho zimetoholewa kwa kuruka ili kuchopokea adui. Pedipalpi zao zina gando. Hawana macho lakini spishi kadhaa zina sehemu za kuhisi nuru.

Takriban spishi zote zinatokea kanda za tropiki. Zinaishi katika tabaka la juu la udongo au chini ya magogo na mawe ili kuzuia kukauka. Spishi kadhaa zinaishi katika mapango na nyingine katika vichuguu. Hula arithropodi wadogo.

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Nge-mjeledi mkia-mfupi: Brief Summary ( Swahili )