Nyoka laini ni nyoka wa jenasi Meizodon katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu ya ngozi yao laini.
Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 80 kwa kipeo lakini sm 30-60 kwa kawaida. Rangi ya wapevu ni kijivu au kahawia lakini nyoka laini kichwa-cheusi ni mwekundu au pinki wenye kichwa cheusi na shingo yenye mkufu mweusi. Wachanga ni kijivu au hudhurungi na kwa kawaida wana mabaka meusi angalau kichwani au kwa nusu ya mbele ya mwili pia.
Nyoka laini hukiakia mchana na hula mijusi, vyura na wagugunaji wadogo.
Nyoka hawa hawana sumu na wanaweza kukamatwa bila shida kwa sababu hawang'ati kwa kawaida.