Mkunde (Vigna unguiculata) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae (miharagwe). Mmea huu hupandwa sana katika Afrika na katika Amerika ya Kati na ya Kusini, Asia na Ulaya ya Kusini pia. Majani na mbegu zake huitwa kunde na hizi ni chakula muhimu.
Nususpishi ya mkunde, mkunde-mwitu (V. u. ssp. cylindrica), hukua porini kwa Afrika lakini hukuzwa pia kama mmea wa mazao na kutoa malisho.
Nususpishi nyingine, mkobwe (V. u. ssp. sesquipedalis), ina makaka marefu sana: sm 35-75 (maana ya "sesquipedalis" ni futi moja na nusu). Makaka hawa au makobwe huliwa kama maharagwe-mboga.