Chati ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Muscicapidae. Siku hizi wataalamu wengi wanaainisha spishi za Thamnolaea katika Myrmecocichla.
Chati hawana rangi kali isipokuwa spishi za Thamnolaea ambao wana tumbo jekundu. Wengine ni weusi, wengine wana rangi ya kijivu au kahawia.
Spishi hizi zinatokea Afrika na kadhaa zinatokea Asia ya Magharibi mpaka Uhindi. Kwa kawaida huonekana juu ya miamba, majabali na vilima vya mawe.
Hula wadudu, matunda madogo, mafuta ya wanyama na takataka za kulika za nyumba.
Hulijenga tago lao kwa vitu vyororo kama sufu, manyoya na nyuzinyuzi juu ya uoto mfupi au kati ya mawe. Jike hutaga mayai 3-5.