Milupini (Lupinus spp.) ni mimea ya nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae (miharagwe). Mbegu zao huitwa malupini. Spishi kadhaa hukuzwa ili kuvuna malupini kwa chakula cha watu, k.m. mlupini mweupe, mlupini majani-membamba, mlupini buluu na spishi ya Amerika ya Kusini Lupinus mutabilis. Spishi nyingine hukuzwa kwa malisho ya wanyama, k.m. mlupini mweupe, mlupini majani-membamba na mlupini njano. Lazima malupini yalowekwe katika maji na chumvi kwa muda wa siku kadhaa kabla kuyapika, kwa sababu yana sumu.