dcsimg

Chechele (Monarchidae) ( Swahili )

provided by wikipedia emerging languages

Chechele ni ndege wa familia Monarchidae. Kuna chechele wengine katika familia Stenostiridae. Zamani walikuwamo katika Monarchidae, lakini uchunguzi wa ADN umeonyesha kwamba hawana mnasaba na ndege hawa na wamepewa familia yao.

Chechele wa Monarchidae wana rangi kali, buluu na nyekundu hasa lakini njano pia; wengine ni weusi na weupe tu. Dume la spishi nyingi ana mkia mrefu sana. Wanatokea Afrika, Asia, Australia na visiwa vya Pasifiki. Spishi nyingi sana zinaishi msituni au katika maeneo yenye miti mingi, spishi chache katika savana kavu. Chechele hula wadudu ambao hukamata kama shore. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini. Mara nyingi huweka kuvumwani katika tago. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi za Afrika

Spishi za Asia

Picha

license
cc-by-sa-3.0
copyright
Waandishi wa Wikipedia na wahariri

Chechele (Monarchidae): Brief Summary ( Swahili )