Ngurunguru au mbuzi mawe (Oreotragus oreotragus) ni swala wadogo wanaotokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Jina “mbuzi mawe” ni kielekezi cha makazi yao: maeneo yenye mawe na majabali mengi. Swala hawa ni wadogo wenye kimo cha sm 58 begani. Wana rangi ya kahawa hadi kijivu, karibu na zaituni, na vidoa vidogo vingi. Rangi hii inafanana na rangi ya majabali ambapo wanaishi na kwa sababu ya hii hawaonekani vizuri kutoka umbali mkubwa. Madume wana pembe za sm 10–15. Katika Afrika ya Mashariki majike wana pembe pia mara nyingi. Wanyama hawa wasimama kwa ncha za kwato zao na wanaweza kubana kwato nne zote juu ya kipande cha jabali kwa upana wa sarafu kubwa. Hula mimea inayomea kati ya majabali. Hawana haja ya kunywa, kwa sababu hupata maji ya kutosha kutoka chakula chao.
Siku hizi nususpishi O. o. porteousi inafahamika tu.
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.